March 31, 2017


Stand United wamefikia kukubali kuwa kweli mambo ni magumu kwao.

Mwenyekiti wa Stand United, Elson Maeja amesema kweli hali ni gumu kwao huku akimkumbuka Kocha Patrick Liewig.
“Mambo ni magumu kwa kuwa hatuna wadhamini, unajua tulikuwa na Kocha Liewig ambaye aliondoka baada ya kushindwa kumlipa.

“Hii ilisababisha tushindwe kufanya vizuri baada ya makocha wengine kutofanya vizuri. Lakini kifedha tumeendelea kudorora,” alisema.

Pamoja na Maeja leo kumkumbuka Liewig, wakati anaondoka viongozi wa Stand United walikuwa wakimponda kuwa aende, wao wana uwezo wa kuendelea.

Lakini taarifa zinaeleza kuwa ukata umeikamata Stand United na hasa baada ya Acacia kujiondoa kama wadhamini wakuu.


Acacia walijiondoa baada ya makundi mawili waliokuwa waanzilishi na wale walioamini wana uwezo wa kuiongoza Stand United kuingia wakiitaka timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV