March 31, 2017


Ruvu Shooting wanaamini kesho itakuwa siku ya wao kuwapa joto wenyeji wao Mbeya City.

Shooting watakuwa ugenini dhidi ya Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kesho.

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wanajua mechi yao ya kesho itakuwa ngumu, lakini lazima wawaonyeshe Mbeya City kwa kuwatoa baridi.

"Hapa Mbeya ni baridi sana, sisi kazi yetu itakuwa ni kuwatoa baridi hawa ndugu zetu," alisema.

"Kikosi chetu kipo vizuri na maandalizi yako safi, hivyo ni kazi yetu kuwapa joto hawa jamaa."

Ruvu Shooting inashuka dimbani kuivaa Mbeya City iliyo katika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV