MO DEWJI AKIWA MAKAO MAKUU YA JUVENTUS NCHINI ITALIA. |
Bilionea kijana zaidi barani Afrika, Mohammed Dewji maarufu kama Mo, ametua nchini Italia na kufanya ziara katika klabu bingwa ya nchini humo, Juventus.
Juventus maarufu kama "Vibibi Kizee vya Turin", ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi kwa kipindi zaidi nchini humo licha ya kuwepo kwa timu nyingine za AC Milan na Inter Milan ambazo zinaonekana kudorora.
Akizungumza kutoka Turin, Italia, Mo Dewji ameiambia SALEHJEMBE kwamba alifanya ziara hiyo na Juventus wameonekana wako tayari kuendeleza mchezo wa soka kwa kuwekeza nchini Tanzania.
“Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo,” alisema Mo.
MO DEWJI AKIWA NA CAROLINA CHIAPPERO, MMOJA WA MAOFISA WA JUVENTUS KATIKA MASUALA YA AKADEMI NA BRANDI.
|
Mo alisema mambo mengi waliyozungumza ni mchakato, hivyo ni suala la kuangalia na huenda atazungumzia zaidi hapo baadaye.
Juventus ni moja ya klabu yenye mfumo bora kabisa wa ukuzaji wa wachezaji vijana. Pia inashirikiana na baadhi ya klabu kubwa za barani Afrika lakini nyingi ni zile kutoka Afrika Kaskazini hasa katika nchi za Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri.
Kama Simba itapata bahati hiyo, itakuwa imepata nafasi nzuri ya kujiendeleza na kujifunza mengi kibiashara na kimaendeleo kupitia Juventus, pia maarufu kama Juve.
Mfanyabiashara huyo ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd, ni mwanachama, shabiki na aliwahi kuwa mfadhili wa Simba kwa kipindi kirefu cha mafanikio.
Lakini kwa sasa, Mo Dewji ameendelea kuifadhiri Simba na imeelezwa kila mwezi amekuwa takribani au zaidi Sh milioni 100 katika ulipaji mishahara na mambo mengine ya motisha kwa wachezaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment