March 30, 2017


Baadhi ya mashabiki wa Simba waliokuwa njiani kwenda Bukoba kuishangilia timu yao wamekutana na dhahama ya ajali baada ya basi walilokuwa wamepanda kupinduka.

Imeelezwa basi hilo limepinduka mkoani Morogoro lakini kati yao, walipata majeraha madogo na kukimbizwa hospitali mkoani hapo.

Taarifa zinaeleza, mashabiki hao wanaendelea vizuri na mmoja wao ni Makoye Nzungu, mmoja wa mashabiki maarufu wa Simba.


Simba inashuka dimbani Jumapili kuivaa Kagera Sugar katika moja ya michezo sita muhimu iliyobaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV