March 28, 2017


Nahodha wa Argentina, Lionel Messi amefungiwa kuichezea timu yake ya taifa kwa mechi nne.

Messi amefungiwa baada ya kumtukana mwamuzi katika mechi dhidi ya Chile ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.

Shirikisho la Soka la KImataifa (Fifa), limewataarifu Argentina ikiwa ni saa sita tu kabla ya kuivaa Bolivia katika mechi muhimu ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

Messi amepatikana na hatia ya kumtukana mwamuzi wa pembeni, Marcelo van Gasse akimtukana yeye na kumtukania mama yake.

Messi ndiye aliyefunga bao pekee lililoipa Argentina ushindi huo wa bao 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV