March 28, 2017


Bosi wa Chelsea, Antonio Conte si mtu wa kujivunga hata kidogo, tayari ameweka hadharani kwamba anamtaka mshambuliaji Alexis Sanchez.

Sanchez ameeleza wazi kwamba anataka kuondoka Arsenal ingawa hajasema anakwenda wapi.

Lakini ajabu, Arsenal inaonyesha haitaki kumuuza London kwa Chelsea au England kwa timu yoyote.

Badala yake, Arsenal inaamini Sanchez anapaswa kuuzwa nje ya England.Conte anaamini, baada ya Chelsea kubeba ubingwa kama mambo yataenda safi hadi mwisho, bass Sanchez atakuwa msaada mkubwa hapo baadaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV