March 27, 2017Kocha Mkuu wa Azam, Mromania, Aristica Cioaba, ameweka hadharani mikakati yake ndani ya timu hiyo katika michezo sita ya Ligi kuu Bara iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu.  

Azam inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 44, imebakiwa na michezo sita ambayo ni sawa na dakika 540 ambapo itapambana na Yanga, Mtibwa, JKT Ruvu, Mbao, Toto Africans na Kagera Sugar.


Cioaba ambaye amepewa mkataba wa miezi sita ndani ya Azam utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu, amesema mechi hizo sita kwao ni kama fainali kwani wanataka kumaliza ligi wakiwa ndani ya tatu bora.

“Kwa sasa tunajipanga kuhakikisha tunashinda mechi zote sita zilizosalia na tuna kila sababu ya kufanya hivyo baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.


“Licha ya kikosi changu kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara lakini kuna mikakati nimeiweka ambayo naamini itatukwamua kwenye hali hii ngumu na kufikia malengo yetu,” alisema Cioaba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV