March 27, 2017


Kituo cha Azam TV, kitaendeleza uhondo wa Ligi Kuu Hispania kwa mechi zake kuonyeshwa moja kwa moja.

Mechi kati ya Real Betis dhidi ya Espanyol, moja ya timu maarufu kwa kutandaza soka safi na zinajulikana kama “kiboko cha vigogo” zitakutana. Mechi hiyo itapigwa Saa 3:45 usiku, Ijumaa hii.


Azam TV, itarusha moja kwa moja mechi hiyo kwa lugha ya Kiswahili.

Espanyol ndiyo watakaokuwa nyumbani dhidi ya Betis ambao ni wabishi wengine na kawaida ni moja ya mechi ambazo hazikutanishi vigogo kama Real Madrid na Barcelona lakini huwa na mvuto mkubwa nchini humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV