March 28, 2017
Real Madrid imeanzisha “Oparesheni Eden Hazard”, ‘yaani iwe isiwe, lazima apatikane!

Kinachoonekana Madrid iko tayari kumwaga hadi pauni million 100 na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani lakini lazima imnase Mbelgiji huyo tegemeo la Chelsea.

Chelsea inaonekana iko kimya na inasubiri ofa na atakayetokea na kisu kikali, ndiye atampata.

Hazard mwenye umri wa miaka 26, sasa ndiye tegemeo kwenye safu ya ushambulizi ya Madrid.


Taarifa la gazeti la AS la Hispania zinaeleza, Kocha Zinedine Zidane anavutiwa sana na Hazard, hivyo iwe itakavyokuwa ni lazima kiungo huyo akaongeze nguvu Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV