March 28, 2017


Kama ilivyo ada ya kituo cha runinga cha Azam TV, leo kitarusha moja kwa moja au mubasharaaa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars itakayokuwa inaivaa Burundi.

Mechi hiyo itakayoanza Saa 10 jioni, inayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, itaonyeshwa na AzamTwo, kwa ubora wa juu au HD na kutoa nafasi kwa mashabiki kwa wigo mkubwa kushuhudia.


Hata hivyo, watakaofaidika na mubashara hiyo ni wale wateja wa ving’amuzi vya Azam TV vilivyolipiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV