March 31, 2017Unamkumbuka Mbuyu Twite aliyewahi kukipiga Yanga akitokea APR ya Rwanda? Ametoa ushauri kwa klabu ya hiyo ya zamani.

Twite yuko Fanja FC ya Oman, ambako anaendelea kuitumikia katika ligi kuu ya nchi hiyo huku akisema anafuatilia kwa karibu Ligi Kuu Bara.

Twite ambaye anajua Yanga itaifaa Azam FC katika mechi ngumu Jumamosi, ametaka wasikate tamaa kwa kuwa lolote linaweza kutokea.

Beki na kiungo huyo, anaamini Yanga bado ina nafasi kubwa ya kuwa bingwa tena.

“Nipo huku lakini naifuatilia ligi ya Tanzania kupitia mitandao mbalimbali, najua Simba wanaongoza wakifuatiwa na Yanga, japo bado mechi zimesalia chache ligi imalizike.

"Lakini naamini lolote linaweza kutokea kati ya timu hizi mbili na si kusema sasa aliye juu anaweza kuwa bingwa kwani anaweza kushushwa na kumaliza akiwa wa pili.

“Tangu nifike huku, nimekutana na ugumu ambao sikuutarajia, nina siku chache huku lakini tayari nimeona tofauti kubwa ya ligi ya Tanzania na ya Oman, lakini kitu kizuri ni kwamba nimeweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza japo ugumu wake si sawa na Tanzania,” alisema Twite.

SOURCE: CHAMPIONI0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV