March 30, 2017


Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kweli suala la taarifa ya nyasi zao bandia kutaka kupigwa mnada, limewashitua sana.

Lakini akawataka mashabiki na wanachama wa Simba kutulia wakati uongozi unapambana katika suala hilo.

“Tokea nyasi hizi zimepita tulifanya juhudi ya kuomba msamaha kwa serikali, unajua nyasi hizi si kwa Simba pekee. Ni kwa kwa jamii yote kwa kuwa tunalenga kuendelea vijana ambao hawatakuwa faida yetu pekee.

“Lakini tumekuwa tukiendelea kupambana kuzitoa, tulishaanza ujenzi wa uwanja na suala la nyasi tu.

“Kuhusiana na taarifa kwamba zinataka kupigwa mnada, kweli linashitua. Unajua kawaida mzigo wako ukikaa bandarini baada ya siku 60, unapewa taarifa ya kupigwa mnada. Tunaendelea kulishughulikia hili,” alisema Kaburu.

Taarifa za Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za Simba imesambaa kwa kasi leo asubuhi.

Imeelezwa kuwa nyasi hizo zitapigwa mnada leo nyuma ya "The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar”.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV