March 30, 2017


Kuna taarifa ya nyasi za bandia za Simba kutaka kupigwa mnada imekuwa ikisamabaa kwa kasi kubwa mitandaoni na iko hivi.

"Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za SIMBA SPORTS CLUB na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia kodi. 

Mnada utafanyika siku ya:
Alhamisi 30/03/2017. 

Eneo:Nyuma ya "The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar", barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa LW9.

Juhudi za kuwasaka viongozi wa Simba ili walizungumzie hili zinaendelea. Baadhi yao bado hawajapokea simu na wengine tunaendelea kuwatafuta. 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV