April 8, 2017


Azam FC imesema itaendelea kumtumia kipa Aishi Manula badala ya Mwadini Ally kwani Manula anaendelea kufanya vizuri kila anapocheza.

Kwa muda mrefu sasa, Mwadini aliyekuwa kipa namba moja amekuwa akikaa benchi na kuacha nafasi kwa Manula ambaye pia ni kipa wa Taifa Stars.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba amesema kuwa: “Mwadini ni kipa wetu mkongwe na ndiye aliyempa uzoefu Manula, lakini leo yupo benchi.


“Mwadini anakaa benchi kutokana na Manula kuwa anafanya vizuri, hatuangushi, lakini uwepo wa Mwadini katika benchi unamfanya Manula aendelee kuwa mzuri na hatumaanishi kama (Mwadini) hafai.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV