Huku akichangia kuipeleka Yanga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho, mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa juzi Jumamosi alipiga vichwa vinne kwenye goli la wapinzani wao Tanzania Prisons huku akifanikiwa kufunga bao moja kwa kichwa.
Mshambuliaji huyo anayenyoa staili ya upara, aliifungia bao hilo dakika ya 40 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Haji Mwinyi.
Mechi hiyo, ilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-0, mawili yakifungwa na Amissi Tambwe pamoja na Simon Msuva.
Wakati mechi hiyo inaendelea, Chirwa alipiga vichwa vingine dakika ya 10, 32 na 71 huku mipira hiyo ikienda nje na kuanzishwa na kipa wa Prisons, Andrew Ntala. Ukipiga hesabu tangu alipopiga kichwa cha kwanza hadi cha mwisho, utabaini alitumia dakika 61.
Katika mchezo huo, mshambuliaji huyo alionekana kuisumbua safu ya ulinzi ya Prisons iliyoongozwa na Salum Kimenya, Leonsi Mutalemwa na James Mwasote.
Chirwa, alishindwa kumalizia mchezo huo baada ya kutolewa dakika 82 na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin baada ya kugongana na kipa aliyeingia badala ya Andrew Ntala, Aron Kalambo na kusababisha ashindwe kuendelea na mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment