April 26, 2017




Mshambuliaji Diego Costa wa Chelsea, jana alifunga bao la 50 akiwa na kikosi hicho chino ya Kocha, Antonio Conte.

Costa alifunga mabao mawili wakati Chelsea ikiitwanga Southampton kwa mabao 4-2 katika mechi ya Ligi Kuu England kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London.

Wakati anafunga mabao hayo mawili, Costa alikuwa anaandamwa na ukame wa kupachika mabao baada ya kucheza mechi tano bila kufunga hata bao moja.

Costa hakuwa amewahi kucheza mechi tano bila kufunga tokea msimu wa 2012-13 alipocheza mechi sita bila kufunga hata bao moja katika La Liga akiwa na Atletico Madrid.

Imemchukua mechi 85 kufikisha mabao 50 ya Ligi Kuu England.

Wengine ambao waliowahi kufunga mabao 50 ya Ligi Kuu England na mechi walizocheza kwenye mabao huku Any Cole akiwa ndiye aliyefunga mabao 50 katika mechi chache au haraka zaidi.

 Andy Cole (65) 
Alan Shearer (66)
Ruud van Nistelrooy (68)
Fernando Torres (72)
Sergio Aguero (81) 
Thierry Henry (83) 
 Kevin Phillips (83)


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic