KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, raia wa Msumbiji amefunguka kwamba ataendelea na kazi ya kutengeneza mabao kwa wenzake ili kuifanya timu hiyo iendelee kupata pointi tatu kwenye mechi zake.
Miquissone ameongeza kwamba licha ya kutoa assisti hizo kwa wenzake lakini pia atafunga kwa sababu ni wajibu wake kikosini hapo.
Miquissone kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu huu amehusika katika mabao sita ya Simba akitoa assisti tano na kufunga bao moja dhidi ya JKT Tanzania.
Miquissone ambaye wengi hupenda kumuita Konde Boy amesema kwamba atahakikisha anaifanya kazi hiyo ya kutoa pasi za kufunga kwa wenzake kwa sababu ni sehemu ya majukumu yake ndani ya kikosi hicho kinachofundishwa na Mbelgiji Sven Vanden broeck.
“Najisikia vizuri kufunga na kutoa assisti kwa wenzangu kwa sababu ni sehemu ya kazi yangu, najua nina uwezo wa kupafomu vizuri.
“Nafanya kazi kuisaidia timu yangu iende juu zaidi ya hapa. Nimefunga bao zuri na kutoa assisti lakini nataka kufunga zaidi,” amesema.
Simba ikiwa imecheza mechi tano imekusanya pointi 13, imefunga jumla ya mabao 14 na kufungwa mabao mawili.
GOOD BWOY
ReplyDeleteNjo vile tunatakaga
Tunapenda hivyo na moto uwaxhe zaidi ya hapo
ReplyDelete