April 7, 2017
Kamati ya saa 72 imefikia uamuzi kuwa ile rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar, itasikilizwa tena Alhamisi.Rufaa hiyo itasikilizwa na kuna asilimia kubwa itatolewa uamuzi siku hiyo ya Alhamisi.


Simba imekata rufaa katika Bodi ya Ligi ikitaka ipewe pointi tatu baada ya kugundua beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano.


Simba walipoteza mechi hiyo Jumapili iliyopita mjini Bukoba kwa kufungwa mabao 2-1.


Kikao hicho cha kusikiliza masuala kadhaa, likiwemo hilo la rufaa ya Simba, kilianza leo saa 9 Alasiri.


Hata hivyo, mwisho kimeshindwa kutoa jibu na kuacha watu na maswali mengi.


Katika mitandao mbalimbali, suala hilo lilizuia gumzo kubwa, wako wakiunga mkono kutaka sheria ifuate mkodo na wengine walikuwa wakipinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV