April 9, 2017
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, ilifanya kikao chake juzi Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao. Mechi namba 12 (Transit Camp 1 vs Cosmopolitan 1). Daktari wa Cosmopolitan, Najim Mtoro amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kumtukana Mwamuzi wa Akiba.


KUPITIA MATUKIO YA LIGI DARAJA LA PILI (SDL Play Off)
Mechi namba 7 (Mawenzi Market 2 vs Transit Camp 0). Klabu ya Transit Camp imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) baada ya timu yake kuchelewa uwanjani kwa dakika 45 katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 18, 2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Adhabu dhidi ya Transit Camp imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(1) na 14(47) kuhusu Taratibu za Mchezo.


Kocha Msaidizi wa Transit Camp, Thomas Gama amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutolewa nje na Mwamuzi katika mchezo kutokana na kumtolea maneno ya kashfa Mwamuzi Msaidizi Namba Moja.


Mechi namba 8 (JKT Oljoro 1 vs Cosmopolitan 0). Klabu ya Cosmopolitan iliwasilisha malalamiko kuwa mechi hiyo iliyofanyika Machi 20,2017 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha ilichezeshwa na Mwamuzi wa Arusha, badala ya Mwamuzi kutoka Singida aliyekuwa amepangwa awali.


Kamati imetupa malalamiko hayo kwa vile si ya kweli, na Mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo alitoka Mkoa wa Manyara, na si Arusha kama walivyodai katika malalamiko yao.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV