April 9, 2017
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72, ilifanya kikao chake juzi Ijumaa Aprili 7, 2017 jijini Dar es Salaam na kufikia uamuzi ufuatao. 

Kuhusu kupulizwa dawa vyumbani Uwanja wa Kambarage
Daktari wa Uwanja wa Kambarage, Dk. Abel Kimuntu amekataa kuwasilisha taarifa yake kuhusu tuhuma za kupuliziwa dawa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Majimaji katika mechi namba 170 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji Stand United. Klabu ya Majimaji iliwasilisha malalamiko yake kwa Bodi ya Ligi kuhusu suala hilo.


Hivyo, Kamati imeagiza suala la daktari huyo lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya hatua za kinidhamu dhidi yake kutokana na kukataa kutoa ushirikiano kwa mwendeshaji wa Ligi juu ya jambo hilo. Kamati ya Nidhamu inatarajiwa kukaa wakati wowote wiki ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV