April 9, 2017


Kiungo Mehd Kaceem wa MC Alger, amesema beki wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy alikuwa mwiba mkali kwao.


Yanga imeitwanga MC Alger kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa, jana.


Kaceem amesema, wanaamini kuna mambo mengi ya kuyafanyia kazi zikiwemo ‘move’ za Kessy.


“Umbo lake ni dogo lakini alikuwa na madhahara makubwa. Umeona krosi zake na pia alipita kutengeneza mipira mingi pembeni,” alisema.


“Tumeona na kocha na wenzake wameona, tuwaachie na sisi tutajua cha kufanya,” alisema kwa lugha ya Kifaransa.

Kessy alionyesha uwezo mzuri katika mechi hiyo ya jana na mara kadhaa alikuwa akipiga krosi zinazowapa wakati mgumu MC Alger.


Yanga walipoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa. Sasa wanajiandaa na mechi ya pili wakiwa ugenini Algers dhidi ya wenyeji wao hao MC Alger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV