April 18, 2017Mchezaji Venance Ludovic ameidhinishwa kuwa mchezaji halali wa African Lyon.

 Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imepitisha uamuzi huo leo katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Lakini Lyon wamepigwa faini ya Sh 500,000 kutokana na kuonekana kuwa hawakufuata utaratibu katika usajili wake.

Mchezaji huyo alikuwa akilalamikiwa kwamba hakukamilisha usajili wakati anajiunga Lyon akitokea Mbao FC.

Lakini yeye alilalamika kwamba Mbao FC walivunja mkataba kwa kushindwa kumyima stahiki zake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV