April 13, 2017



Wakati taarifa zimekuwa zikisambaa mitandaoni kuwa tayari Simba wameshinda rufaa yao na kupewa pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar, ukweli ni kwamba kikao cha kamati ya Saa 72, kitakaa saa 9 Alasiri jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kitakaa leo hii na kuamua kuhusiana na rufaa hiyo ya Simba inayolalamika mchezaji Mohamed Fakhi kuwa na kadi tatu za njano.

Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Bukoba, Simba ililala kwa mabao 2-1.

Lakini kuanzia muda mchache uliopita, taarifa zimekuwa zikisambaa mtandaoni kwamba tayari kikao kimekaa na Simba wamepewa pointi tatu.

"Kikao bado, itakuwa saa 9, hao wanaosema nafikiri wanazusha tu mambo," alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

"Watuache tufanye kazi yetu, wasilazimishe mambo na kutaka kuleta mkanganyiko."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic