April 3, 2017Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema anaamini kikosi chake kitaendelea kuimarika katika mechi zijazo.

Lwandamina amesema, anaamini kikosi kitaimarika kutokana na wachezaji wake kuanza kupata ahueni.

Yanga imekuwa ikiandamwa na majaruhi wakiwemo wachezaji tegemeo kama Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko.

"Kadiri siku zinavyosonga mbele, mambo yatabadilika. Muda ukisonga, watakuwa wakipona na kurejea," alisema.

"Kila watakavyokuwa wakirejea, basi tutaendelea kuimarika kulingana kikosi kuimarika zaidi," alisema.

Pamoja na kuwa na majeruhi tena wachezaji wake walio muhimu, lakini Yanga ilifanikiwa kuitwanga Azam FC kwa bao 1-0 na kutinga kileleni mwa Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV