April 4, 2017Bondia mstaafu, Floyd Mayweather ameendeleza nyodo ya fedha baada ya kumwaga kitita cha sh milioni 84 ambazo ni pauni 31,000 kununua gari la zawadi.

Mayweather maarufu kama Money, amenunua gari aina ya  Mercedes C-Class Coupe kwa ajili ya mwanaye Zion ambaye ametimiza miaka 16.

Pamoja na gari hilo la kifahari, wasanii kadhaa maarufu walitumbuiza katika pati hiyo ya siku ya kuzaliwa ya Zion huku yeye akiwa anamwaga fedha kama ilivyozoeleka kwa baba yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV