April 7, 2017Pamoja na kipigo kutoka kwa Kagera Sugar, Simba wametamba kuwa haijawaathiri kisaikolojia badala yake wamelichukulia suala hilo kama la kimichezo.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanaendelea na maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwa mipango sahihi.

“Kufungwa si kitu kizuri, lakini haina maana kwamba suala hilo limetuchanganya.

“Naweza kukuhakikishia vijana wako vizuri tayari kwa mchezo ujao na kurekebisha makosa,” alisema.

“Mchezo ujao utakuwa muhimu zaidi ya mchezo wa awali. Tunataka kufanya vizuri na hili liko kwa wachezaji, makocha na kila mmoja wetu.”


Simba ilifungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar mjini Bukoba Jumapili iliyopita hali iliyosababisha ishushwe kileleni baada ya Yanga kuwa imeishaichapa Azam FC kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV