April 10, 2017



Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, amesema baada ya kikosi hicho kukaa kwenye usukani wa ligi kwa sasa lengo lao lililobakia ni kuhakikisha wanashinda kwenye mechi zao zote ili waweze kuwa mabingwa.

Yanga wamejikusanyia pointi 56 baada ya kushuka dimbani mara 25, pointi ambazo zinawafanya wawe juu ya timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara huku Simba wenyewe wakikamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 55.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao tisa mpaka sasa kwenye ligi, amesema kwamba kwa muda mrefu Simba walijiaminisha kwamba wanachukua ubingwa wakasahau kuhusu wao ambao walikuwa wanazisuka mbinu zao kimyakimya.

“Kilichobakia kwa sasa ni kuhakikisha kwamba tunashinda kwenye mechi zetu tano zilizobakia kwa ajili ya kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa wetu ambao tulikuwa tunaupigania kwa nguvu kubwa.

“Niwaambie nafasi hii tuliyonayo kwa sasa ndiyo tumemaliza kila kitu kwani hatutaki kuona tukirejea kwenye nafasi tuliyokuwa awali na nawaomba wenzangu tushirikiane vyema katika kushinda mechi hizi zilizobakia,” alisema Tambwe.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV