April 10, 2017



KIKOSI cha Mbeya City, kimeshindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano mfululizo ambayo ni sawa na dakika 450 hali ambayo inaiweka njia panda timu hiyo kwenye harakati zao za kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo ambayo juzi Jumamosi ilifungwa mabao 2-1 na Ndanda wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya, mwanzoni mwa msimu huu iliweka mikakati ya kumaliza ligi ndani ya timu tano bora za juu.

Mbeya City kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 32, mara ya mwisho kupata ushindi kwenye michezo yake ya Ligi Kuu Bara ilikuwa ni Februari 5, mwaka huu walipoifunga JKT Ruvu bao 1-0, lakini baada ya hapo wamecheza mechi tano na kushindwa kupata ushindi.

Matokeo ya mechi hizo yalikuwa hivi; Mwadui 3-2 Mbeya City, Stand United 0-0 Mbeya City, Simba 2-2 Mbeya City, Mbeya City 1-1 Ruvu Shooting na Mbeya City 1-2 Ndanda ambapo wamekusanya pointi tatu kati ya pointi 15.

Kutokana na hali hiyo, kocha wa kikosi hicho, Kinnah Phiri, raia wa Malawi, amesema: “Matokeo si mazuri sana, lakini tunaendelea kupambana kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea, hali hii inaweza kuitokea timu yoyote ile na hiyo ndiyo maana halisi ya mchezo wa soka, matokeo ya kushangaza ni sehemu mojawapo ya changamoto.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic