May 25, 2017





Kocha Bora wa Ligi Kuu Bara, Mecky Maxime amesema ni kazi ngumu kwa timu ya mkoani kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Maxime ambaye ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, amesema kumekuwa na figisu nyingi katika soka nchini hali inayotoa nafasi kwa Yanga na Simba kuendelea kutamba.

“Niamini, ni kazi ngumu sana kwa timu za mikoani kuchukua ubingwa kutokana na mizengwe,” alisema Maxime wakati akihojiwa na kipindi cha SPOTI HAUSI katika Global TV Online.

Maxime amesema pamoja na hivyo amekuwa na ndoto ya kufanya vizuri zaidi ikiwezekana kupanda kutoka katika nafasi ya tatu hadi ya pili au ubingwa.

“Kweli nataka kwenda juu zaidi na ikiwezekana nibebe ubingwa. Lakini sijui,” alisema.


Maxime amewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili akiwa na Mtibwa Sugar kama mchezaji. Wakati huo alikuwa akicheza beki ya kulia.

1 COMMENTS:

  1. Wakati zinachukua ubingwa Mtibwa,Tukuyu, Prisons, Mseto,Reli, Pamba ....... Yanga na simba sc hazikuwepo?? Au hzo ffitina na mizengwe imekuja wakt yeye amekuwa kocha au imeanza miaka ya hv karbun...? Mexime nae amekuwa na maneno mengi mno afundishe timu ikiwa nzr ubingwa atachukua tu....na kama anaona Tz ni figisu kuchukua ubingwa aende akafundishe nje ya nchi kenya uganda ethiopia au hata south africa huko nahisi hakuna mizengwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic