May 9, 2017


Baada ya kusubiri kwa hamu, hatimaye kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa imezinduliwa nchini leo.

Sasa ni rasmi SportPesa imezinduliwa hapa nyumbani katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Uzinduzi wake pia ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanamichezo, wasanii na wanahabari.


Kampuni hii ni mpya kwa maana haikuwa hapa nyumbani, lakini ndiyo maarufu zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na imekuwa ikifanya kazi zake nchini Kenya na watu wakijishindia mabilioni ya fedha.

Hali hiyo imefanya watu wengi wanaopenda michezo hiyo ya kubashiri kutamani siku moja SportPesa ianza kazi hapa nyumbani.

Sasa leo ndiyo siku yenyewe wakati SportPesa itakapozinduliwa rasmi hapa nchini.


Taarifa za uhakika kutoka jijini Dar es Salaam zinaeleza, SportPesa itazinduliwa leo rasmi.


SportPesa imekuwa maarufu si kwa ajili ya kubeti tu, lakini ni kampuni ambayo imekuwa ikirejesha fedha inazopata katika jamii.

Nchini Kenya kwa kiasi kikubwa imesaidia kurejea kwa ushindani wa Ligi Kuu ya Kenya baada ya kuidhamini.

Kama haitoshi, SportPesa imewadhamini wakongwe wa soka la Kenya Gor Mahia na AFC Leopards na kusababisha kurudisha kwa ushindani dhidi yao.


Lakini wameendelea kutanua mipaka kwa kudhamini timu kadhaa za Ligi Kuu England kama Hull City, Southampton na Arsenal jambo linalowafanya kwua kampuni hasa ya michezo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV