May 9, 2017





MPIRA UMEKWISHAAAAAA
Dk 90, Yanga wanaonekana kuupoza mpira zaidi
KADI Dk 87, Mbaraka Yusuf analambwa kadi nyekundu hapa. Anatoka nje hapa, inaonekana alishindwa kuzithibiti hasira zake


Dk 85 sasa, Yondani yuko chini anatibiwa pale baada ya kupata dhoruba
Dk 82, Fakhi analala na kuokoa mbele ya Msuva na kuwa kona, inachongwa lakini haina msaada
 SUB Dk 78 Chirwa anakwenda benchi upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony
Dk 76 kwa mara nyingine, Kaseja anaonyesha umahiri wa juu kabisa baada ya kuruka na kudaka vizuri kabisa hapa kichwa kilichopigwa vizuri kabisa hapa na Tambwe
Dk 74 Mbaraka Yusuf anaangushwa nje kidogo ya 18 ya Yanga. Kagera wanapiga faulo lakini haina nguvu
Dk 72 Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kabisa lakini Kaseja anaonyesha umahiri hapa, anapangua vizuri kabisa
Dk 69, Mbaraka Yusuph anaachia mkwaju mkali hapa, lakini Yanga wanaokoa na Themi Felix anashindwa kuuthibiti mpira


Dk 68 Ame Ali hapa alikuwa anaingia vizuri lakini anaangushwa hapa na mwamuzi anasema ni faulo
Dk 67 Kaseja analazimika kuukoa mpira kwa kichwa baada ya kutaka kuonyesha manjonjo
Dk 65, Kaseja anadaka hapa mbele ya Tambwe ambaye alikuwa na nafasi nzuri ya kuandika bao la tatu
SUB Dk 64 anatoka Kessy kwa upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Juma Abdul wakati Kagera wamemuingiza Japhet Makarai 'Balotelli' akichukua nafasi ya Edo Christopher
Dk 61, Fakhi na Kaseja walijichanganya hapa na mpira unatoka na kuwa kona


SUB Dk 58 Kagera wanamtoa Babu Seif na nafasi yake inachukuliwa Anthony Matoghola
DK 57, Msuva anachuana vikali hapa na Fakhi hata hivyo anamzuia
Dk 55, Niyonzima anaachia mkwaju mkali hapa lakini Kaseja anadaka kwa ubora kabisa
GOOOOOOOOOO Dk 52, krosi safi kabisa hapa ya Niyonzima, Chirwa anaunganisha vizuri kabisa na kuandika bao la pili
Dk 48, krosi nzuri ya Kessy inatua kwa Msuva lakini anashindwa kuunganisha
Dk 45 Yanga wanaanza kwa kasi kubwa wakionekana wamepania kupata bao la pili 



MAPUMZIKO
-GOOOOOOOOOOOO Mbaraka Yusuf anaachia mkwaju mkali kabisa na kuandika bao safi kwa Kagera 
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yondani analala na kuokoa mpira hapa dhidi ya Ame Ali
Dk 43 Kakolanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju mkali wa Mbaraka Yusuf na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina manufaa
Dk 41 Mwinyi Haji anamuangusha Mangoma ambaye alijaribu kumtoka hapa


GOOOOOOOOOOOO Dk 39 Msuva anaruka na kupiga kichwa safi akiunganisha kona ya Mwashiuya na kuiandikia Yanga bao safi kabisa
Dk 35, Mangoma nje ya 18, anaachia mkwaju mkali hapa, hata hivyo hakulenga lango
Dk 31, Fakhi anautoa mpira nje tena na kuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, Mwashiuya anajaribu kufanya yake lakini anakosea
Dk 30 Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini hakuwa amelenga lango


Dk 26 sasa, Yanga wanaonekana kujipanga vizuri kupeleka mashambulizi mengi lakini Kagera Sugar wanaonekana wakiwatuliza Yanga
Dk 22, Yanga wanapata koa nyingine baada Mangoma kupiga fyongo. Inachongwa kona lakini Kagera wako makini
Dk 20, Chirwa akiwa ndani ya hatua tatu, anapiga mpira kabla ya kuingia wavuni unaokoleewa na Kavila na kuwa kona. Inachongwa lakini Kagera wanaokoa hapa
Dk 16, Fakhi anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa mpira dhidi ya Chirwa na kuwa kona. Inachongwa vizuri lakini Yanga wanaokoa hapa
Dk 15, Mbaraka Yusuf anamtambuka Cannavaro ambaye analazimika kumkinga na kumuangusha. Cannavaro ameonyesha uzoefu wake maana ilikuwa ni hatari


Dk 13, krosi safi ya Kessy, Msuva anaachia bunduki kali, lakini hakulenga lango. ilikuwa hatari hapa
 Dk 10 sasa, Kaseja yuko chini pale akitibiwa. Inaonekana alipata maumivu wakati akijaribu kuokoa
Dk 10, Yanga wanafanya shambulizi jingine kali kabisa hapa, lakini Kaseja anaruka kama nyani na kuokoa, lakini amegongwa na kuanguka chini 
Dk 6, krosi safi ya Kessy hapa lakini Fakhi anaruka vizuri na kuokoa hapa
Dk 4, krosi nzuri ya Niyonzima anajaribu hapa Chirwa lakini inashindikana
Dk 1, Yanga imeanza kwa kasi ikiwa imepania kufunga bao la mapema

1 COMMENTS:

  1. Nawatakia ushindi timu yangu Dar-es-Salaam Young Africans (Yanga,
    My best team ever in Tanzania!I hope this marks our good run to VPL 2016/2017 Trophy

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic