May 9, 2017

Kampuni ya michezo ya kubahatisha SportPesa imezinduliwa leo na moja kwa moja imemwaga Sh milioni 50 kuisaidia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ni jambo zuri kwa SportPesa kuonyesha wanajali kwa kiasi kikubwa na Serengeti Boys inahitaji msaada wa wadau kama ambavyo imefanya kampuni hiyo kutoka Kenya.

Serengeti Boys italiwakilisha taifa la Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika nchini Gabon.

Uzinduzi wa kampuni maarufu ya michezo  kubahatisha ya SportPesa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, uliwakutanisha wadau mbalimbali wa michezo na burudani.


Kampuni hiyo imeahidi kusaidia mambo mbalimbali katika udhamini wa michezo hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kusaidia mabadiliko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV