May 9, 2017


Wachezaji wawili wa Real Madrid, Isco na Karim Benzema wamebainika walionyesha nidhamu kwa makusudi dhidi ya Kocha wa Granada, Tony Adams.

Adams alikuwa nahodha wa Arsenal ambayo ilipata mafanikio makubwa nchini England.

Sasa ni kocha wa Granada na timu yake ilikuwa ikicheza dhidi ya Real Madrid na kuchapwa mabao 4-0 katika mechi ya La Liga hivi karibuni.

Lakini Benzema amebainika alikuwa wa kwanza kuhoji mavazi ya Adams, wakati akwa katika benchi.

Mbaya zaidi, Isco akaamua kumuita Adams kama mhudumu kutokana na muonekano wa mavazi yake.

“Haloo, mhudumu, leta Coca Cola.”


Wasau wengi wameonekana kutokubaliana na walichokionyesha wachezaji hao wa madrid kwamba wameshindwa kuonyesha heshima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV