June 4, 2017Kikosi cha AFC Leopards kutoka Kenya chini ya Kocha Mtanzania, Denis Kitambi kimefanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mazoezi hayo ya AFC ni ya mwisho kabla ya kesho kuanza michuano ya SportsPesa Super Cup dhidi ya Singida United.

Bingwa wa SportsPesa Super Cup atapata nafasi ya kucheza na Everton kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Singida United, inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV