June 4, 2017Mshambuliaji Mrisho Ngassa ataanza kuichezea Yanga katika michuano ya SportsPesa Super Cup kesho.

Yanga itaivaa Tusker FC ya Kenya katika mechi ya pili baada ya Singida United kuwa imeanza mechi ya kwanza dhidi ya AFC Leopards.

Ngassa amefanya mazoezi na Yanga jana na leo asubuhi tayari kwa mechi hiyo ya SportsPesa Super Cup.

Taarifa zimeeleza kwa kuwa michuano hiyo wachezaji huru wanaweza kushiriki, Yanga imeamua kumtumia Ngassa baada ya yeye kuomba kwa kuwa ni mchezaji huru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV