June 6, 2017


Bado Cristiano Ronaldo hajamaliza sherehe ya kushangilia ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ametupia mtandaoni video ikimuonyesha akishusha bonge la dansi mbele ya mpenzi wake wakiwa katika ndege.

Ronaldo alikuwa katika ndege pamoja na mpenzi wake na rafiki zake akiendelea kushangilia ubingwa wake wa nne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Real Madrid ilitwaa ubingwa huo kwa kuitwanga Juventus kwa mabao 4-1 huku Ronaldo akifunga mabao mawili.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV