June 1, 2017
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema klabu hiyo haiwezi kumng’ang’ania mchezaji.

Hans Poppe amesema ni vizuri mchezaji anayetaka kuondoka Simba, basi aage vizuri.

“Sisi si tunaoziba riziki. Kumbuka Kaseja aliondoka baada ya kulipwa shilingi milioni hamsini,” alisema katika mahojiano na kipindi ch SPOTI HAUSI kinachorushwa na Global Tv Online.

“Mimi nakerwa sana na mchezaji ambaye anaanza kuzungumza maneno huko wakati tulikaa pamoja. Si vizuri kudanganya wakati huu ni mwezi wa toba.

“Ajibu na Banda wote tumeishazungumza nao, lakini nashangazwa na kusikia wanasema hawajazungumza na viongozi. Huu ni uongozi wenye madhahara pia ni kutaka kuwatengenezea viongozi chuki na mashabiki,” alisema.


Hans Poppe alisisitiza, wachezaji wastaarabu wakati wa kuaga ili kama watashindwa warejee tena Simba badala ya kuzozana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV