June 8, 2017




Michuano ya Ndondo Cup imerejea tena kwa mara nyingine.

Kampuni ya  Azam Media kupitia Azam TV, imeingia makubaliano na waandaaji wa michuano ya Sports Extra Ndondo Cup ya kuonesha michuano hiyo kuanzia hatua ya makundi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Hii ni mara ya nne kwa Azam TV kuonesha michuano hiyo kwani msimu wa kwanza na wa pili, walionesha kuanzia hatua ya nusu fainali mpaka fainali, msimu wa tatu wakaanzia hatua ya 16 Bora.

Mratibu wa michuano hiyo, Shaffih Dauda, amesema: “Hatua ya mtoano itakuwa na timu 32, tunawashukuru Azam TV kwa kukubali tena kuwa nasi kwa msimu mwingine.”

Naye Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, amesema: “Tunapoona kitu kizuri kama hiki huwa tunakuwa haraka kuungana nao kuwasapoti, hivyo basi tumejipanga kuhakikisha michuano ya msimu huu tunaionesha kwa kiwango cha hali ya juu ili wapenda soka wapate burudani.”


Tido aliongeza kuwa, leo Ijumaa Azam TV itaonyesha ‘live’ wakati itakapochezeshwa droo ya hatua ya makundi ya michuano hiyo itakayofanyika saa 9 alasiri kwenye Ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic