June 3, 2017

NDIKUMANA (WA KWANZA KUSHOTO) AKIWA NA KIKOSI CHA MBAO FC.


Mara tatu beki wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana amefanikiwa kumzuia straika wa Simba, Laudit Mavugo asiifunge timu yake, sasa beki huyo amesema Yanga inamtaka na amezungumza nayo.

Katika mechi za Simba na Mbao msimu uliopita, zote Mbao imefungwa ambapo katika Ligi Kuu Bara ilifungwa bao 1-0 kisha 3-2, halafu katika fainali ya Kombe la FA, Simba ikashinda mabao 2-1.

Muzamiru Yassin aliifungia Simba bao pekee katika ushindi wa bao 1-0, halafu Fredric Blagon alifunga mabao mawili na Muzamiru moja katika ushindi wa mabao 3-2, tena Blagnon alifunga bao moja na Shiza Kichuya moja katika fainali ya FA.

Katika mechi zote hizo, Yanga ilikuwa upande wa Mbao ikiishangilia kwa nguvu timu hiyo ili iifunge Simba, lakini sasa imejikuta ikivutiwa na Ndikumana raia wa Burundi ambaye baba yake mzazi ni Mtanzania.

Ndikumana, alisema: “Timu nyingi zinanihitaji lakini Yanga ndiyo niliozungumza nao kwa kirefu na wao wanaonekana wapo makini katika kunisajili.

“Timu nne zilizonifuata ni Simba, Yanga, Azam na Kagera Sugar, lakini siwezi kuamua chochote kwani masuala yangu yote kwa sasa nimemuachia wakala wangu.


“Japokuwa Yanga ipo makini lakini wakala wangu ndiye atakayemalizana nao, na mimi kazi yangu ni kwenda kucheza tu,” alisema Ndikumana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV