July 8, 2017Mshambuliaji Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji kuanzia msimu ujao atavaa jezi namba 10 katika kikosi hicho akiachana na namba 77 aliyokuwa akiivaa tangu alipojiunga nao.

Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, amekuwa akivaa jezi namba 10 pia katika kikosi cha timu ya taifa lakini tangu alipojiunga na Genk mwaka jana amekuwa akivaa jezi namba 77.

Katika taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Genk, kuanzia msimu ujao Samatta atavaa jezi namba 10 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na kiungo mshambuliaji Tino-Sven Susic raia wa Bosnia na Herzegovina.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe na hadi sasa ameichezea mechi 51 na kufunga mabao 17 na amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu hiyo.

Msimu uliopita aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League wakitolewa na Celta de Vigo katika hatua hiyo kwa mabao 4-3 ambapo katika mchezo wa kwanza ilifungwa 3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.


Bado Samatta ni mchezaji wa Genk, japokuwa zimekuwepo tetesi za mshambuliaji huyo kutakiwa na klabu nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV