July 10, 2017




Yanga itaanza mazoezi kujinoa chini ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, kesho.

Hii ni baada ya kusogeza ratiba kwa siku moja baada ya wachezaji wake kadhaa akiwemo Ibrahim Ajibu, Abdallah Shaibu 'Ninja' na Pius Buswita kutofika katika upimani huo wa afya ambao wanafanyiwa wachezaji wote.

Ajibu amejiunga na Yanga hivi karibuni akisaini mkataba wa miaka miwili akitokea Simba baada ya mkataba wake na Mnyama kumalizika mapema mwezi huu.

Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema timu hiyo ilitarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na Ngao ya Jamii na Ligi Kuu Bara leo Jumatatu lakini kutokana na baadhi ya wachezaji kutojitokeza kwenye zoezi la upimaji wa afya zao, kocha ameona asogeze mbele.

Saleh alisema, timu hiyo itaanza mazoezi yake ya pamoja kesho Jumanne asubuhi kwenye uwanja watakaoutangaza mara baada ya kuupata.

Aliongeza kuwa, sababu nyingine ya mazoezi hayo kusogezwa mbele ni kutokana na baadhi ya wachezaji kuchelewa kurejea jijini Dar es Salaam baada ya kwenda likizo.

"Mazoezi rasmi ya pamoja kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii na msimu mpya wa ligi kuu hayatafanyika tena kesho (leo Jumatatu) kama tulivyopanga awali.


“Kocha alitoa maelekezo kwa uongozi kuwa anataka kuona wachezaji wote wanapima afya zao kabla ya kuanza mazoezi na tayari baadhi ya wachezaji wameshapima," alisema Saleh.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic