July 10, 2017Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa angalizo kwa klabu zote za Ligi Kuu Bara kuhakikisha zimekamilisha usajili ifikapo Agosti 6, mwaka huu.

TFF imesema hakutakuwa na nafasi ya kuongeza muda kwa timu yoyote ambayo haitakuwa imekamilisha usajili.

"Muda upo, kila timu inajua na hadi sasa wanajua muda sahihi wa mwisho ni upi," alisema Msemaji wa TFF, Alfred Lucas.

"Hivyo nawapa tahadhari mapema. Hakutakuwa na nafasi tena ya kuongeza muda au kuishawishi Fifa kutupa muda kama ilivyokuwa msimu uliopita.

"Timu ambayo haitakamilisha usajili ndani ya muda, ijue itakuwa imejiteremsha daraja," alisisitiza Alfred.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV