July 9, 2017


Kiungo mwenye kasi wa Simba, Shiza Kichuya amesema michuano ya Cosafa imemuongezea hali ya kujiamini.

Kichuya alikuwa kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika michuano hiyo kwa kuonyesha kiwango bora akiitumikia Tanzania, Taifa Stars iliyoshika nafasi ya tatu.

"Ilikuwa michuano migumu sana, lakini umeona tumecheza kwa ushirikiano na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu. Binafsi nimejifunza na hali ya kujiamini, imeongezeka," alisema.

Kichuya alifanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora katika michuano hiyo. Wengine ni Erasto Nyoni, Muzamiru Yassin na Elius Maguri ambao pia waliibuka wachezaji bora katika mechi nyingine tofauti na kurejea nyumbani na tuzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV