July 9, 2017


Kipa mpya wa Yanga, Youthe Rostand ametamba yuko tayari kwa ushindani katika kikosi hicho.

Kipa huyo aria wa Cameroon amejiunga na mkataba wa miaka miwili na anaamini atapambana na kupata namba.

“Unapojiunga na timu kubwa kama Yanga lazima ujiandae na ushindani ambalo ni jambo zuri,” alisema.

Tayari Yanga ina makipa wawili nyota ingawa, Deogratius Munishi ‘Dida’ ameonyesha nia ya kuondoka na Ally Mustapha ‘Barthez’ akiwa kimya kabisa.

Lakini kipa mwingine, Beno Kakolanya alimaliza msimu akiwa katika kiwango kizuri na kipa huyo mpya anaonekana kuwa tayari.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV