July 19, 2017

Aliyekuwa kocha wa timu ya Geita Gold Mine, Choke Abeid ameachiwa huru kuendelea na shughuli za soka baada ya awali kufungiwa kujihusisha na mchezo huo kutokana na tuhuma za kupanga matokeo.

Akizungumza juu ya uamuzi huo wa kumuachia Choke, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, Rahim Shaban Zuberi amesema kuwa kocha huyo hakuwa na kosa lolote ambalo amelifanya baada ya kumshawishi kipa wa timu ya JKT Kanembwa arudi uwanjani kuendelea kudaka wakati timu hizo zilipokutana msimu wa 2015/16.

Ikumbukwe kuwa Choke akiwa Geita alikuwa ni msaidizi wa Seleman Matola ambaye ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, adhabu yake ilitolewa wakati wa utawala wa Jamal Malinzi ambaye kwa sasa anaelekea kumaliza muda wake na hayumo kwenye orodha ya wanaowania kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa TFF ujao.

“Kama kamati tumekaa na kuliangalia suala la kocha huyo na kubaini kuwa hakuwa na kosa lolote lile baada ya kumshawishi kipa wa wapinzani wao arudi uwanjani kuendelea kucheza, hivyo tunatangaza kwamba yuko huru kutoka kwenye kifungo cha maisha ambaycho alihukumiwa mwanzo.

“Lakini kamati pia ilipitia rufaa za watu wengine ambao walihukumiwa kutojihusisha na soka wakiwemo Yusuph Kitumbo, Fatch Rhemtullah na Thomas Mwita, hawa adhabu yao itaendelea kama ilivyo mwanzo,” alisema.       

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic