Simba Queens waliweka rekodi kwa mara ya kwanza kwa kuwafunga JKT Queens mabao 9-1 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, wakati Yanga Princess waliwachapa 10-0 Allan Queens waliopo Ligi Daraja la Kwanza mchezo ukipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.
Kocha wa JKT Queens, Ally Ally aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tumefungwa dhidi ya timu bora, nawapongeza Simba wamefanya uwekezaji wa wachezaji bora, mimi bado timu yangu ina majeruhi wengi sana kwahiyo ni ngumu kupata matokeo dhidi ya timu bora kama hii.
”Naye kocha wa Allan Queens Mbwana Mbaraka alisema: “Ni ngumu sana kushinda mbele ya timu bora na kubwa kama Yanga, kikubwa ambacho mimi kama mwalimu nafurahia ni kwamba wachezaji wangu wanapata uzoefu wa kucheza na timu kubwa kabla ya kuanza ligi yetu.
”Simba wanatarajia kucheza michezo mingine ya kirafiki wiki ijayo, Jumanne watacheza na Allan Queens huku Jumatano wakikipiga na Ilala Queens michezo yote itapigwa Mo Simba Arena.
STORI: ISSA LIPONDA, Dar es Salaam
0 COMMENTS:
Post a Comment