Kuelekea mchezo huo, uongozi wa timu hiyo umesema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanafanya vema ikiwemo kushinda mechi zote watakazokabiliana nazo huko mbeleni.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari Yanga, Dismas Ten, amesema Yanga hivi sasa inapigania ubingwa wa ligi na popote itakapokuwa na mechi dhumuni lake ni kupata matokeo.
Yanga inashuka dimbani leo kuendeleza safari yake ya kuurejesha ubingwa wa ligi baada ya kuukosa msimu uliopita ulioneda kwa watani zao wa jadi Simba.
Ikumbukwe Yanga ndiyo inayoongoza kuchukua taji hilo kama mabingwa wa kihistoria kwa kuutwaa mara 27 huku Simba wakibeba mara 19.
0 COMMENTS:
Post a Comment