July 15, 2017


Straika aliyejiunga na Azam FC, Mbaraka Yusuf ni kama ameanza na nuksi kwenye timu hiyo baada ya jopo la madaktari kumtaka kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu.

Wachezaji hao waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kikishiriki michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini iliyomalizika hivi karibuni.

Daktari Mkuu wa Azam, Mwanandi Mwankemwa alisema wachezaji wote hao wawili walifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Muelmed, iliyopo mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Alisema kuwa, wachezaji hao baada ya kufanyiwa vipimo Idd aligundulika kuwa misuli miwili ya paja imechanika huku Mbaraka akionekana ana tatizo la Henia.

“Kwa hiyo Shaaban Idd alipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya katika Hospitali ya Muelmed na atatakiwa kupumzika kwa muda wa wiki tatu na baada ya hapo ataanza mazoezi mepesi kuweza kurejea kwenye ushindani.


"Mbaraka yeye madaktari waligundua kuwa baridi ndilo lilikuwa likisumbua na kumsababishia kupata tatizo la Henia itakayomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu naye."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic