July 15, 2017



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema timu yake iko tayari kupambana dhidi ya Rwanda, leo Jumamosi na matumaini yake makubwa ni kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Taifa Stars inacheza mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), dhidi ya Rwanda kwenye Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini hapa.

Mayanga amesema, kutokana na timu yake kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo, imani yake kuwa ni kufanya vizuri dhidi ya Rwanda.

“Timu yangu imefanya mazoezi kwa siku nne mfululizo na maendeleo ni mazuri, tumekubaliana kupambana tuhakikishe tunashinda mchezo huu, ili tuweze kusonga mbele katika michuano hii,” alisema Mayanga.

Katika hatua nyingine, Mayanga amewasifia wachezaji aliowaongeza katika timu yake baada ya kumalizika kwa Michuano ya Cosafa kwa kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani.

“Wachezaji niliowaongeza katika kikosi changu, wanafanya vizuri sana na wana uwezo mkubwa hivyo wameniongezea morali kuelekea mchezo dhidi ya Rwanda kwani uwezo wao uwanjani ni mkubwa," alisema.


Mayanga amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars ikicheza dhidi ya Rwanda maarufu kama Amavubi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic