July 8, 2017



Mgombea pekee wa nafasi ya ukatibu kwenye Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Somoe Ng’itu ameahidi kupambana kuhakikisha soka la wanawake linapiga hatua ikiwa atachaguliwa kwenye nafasi hiyo.

Uchaguzi wa TWFA unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Chichi uliopo wilayani Kindondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar, Ng’itu alisema soka la wanawake limekua lakini bado halijafikia kiwango kile kinachohitajika hivyo kama akipewa nafasi atahakikisha anasaidia kuliinua yeye pamoja na wenzake watakaochaguliwa.

“Nikiwa na mgombea wa nafasi ya ukatibu wa TWFA, ninaona soka la wanawake bado halijafika katika kiwango kile kinachotakiwa hasa kupitia kwenye timu yetu ya wanawake ya Twiga Stars.

“Hivyo, basi katika kuhakikisha tunafikia katika ‘levo’ nzuri ile tunayohitaji ni lazima niwepo kwenye uongozi wa TWFA na ndiyo maana nimeingia kwenye kinyanganyiro hicho cha uchaguzi kwa kuwa ninaamini ninaweza kulikuza soka letu kwa kushirikiana na wenzangu,” alisema Ng’itu.

Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni uenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, katibu msaidizi, mweka hazina, ujumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ujumbe wa kamati ya utendaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic